Mwenyekiti wa (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuachiwa huru yeye pamoja na viongozi wengine sita wa CHADEMA na kusema kuwa walipokuwa magerezani wameshuhudia mengi na watayaweka wazi karibuni.
Mbowe amesema hayo alipokuwa nje ya Mahakama ya Hakimu mzaki Kisutu baada ya kukamilisha masharti dhamana ambapo kila mmoja alitakiwa kuwa na wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilling Million 20.
"Leo mahakama imetupa ruksa ya dhamana na tunaanza dhamana yetu siku ya leo kwa mashtaka ambayo yananikabili mimi na wenzangu, tumekuwa gerezani Segerea kwa siku saba mimi na wenzangu na tunamshukuru Mungu tuko salama mimi na wenzangu na tumewaona Watanzania wengi zaidi ya elfu mbili ndani ya gereza la Segerea ambao wengi wao haki yao imecheleweshwa kwa hiyo tunasema ni haki iliyominywa, tutazungumza mengi tuliyoyaona Segerea na baadaye tutatoa taarifa rasmi ya chama kuhusiana na kesi hii" alisema Mbowe
Aidha Mbowe aliendelea kusema kuwa "Zamani tuliona nchi hii ina udikteta uchwara ila sasa ina udikteta kamili, tutayazungumza na kutolea ufafanuzi kamili katika muda muafaka" alisisitiza
Mbowe Afunguka kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuachiwa Huru
0
April 03, 2018
Tags