Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), imesema haitasoma hotuba wala taarifa zake bungeni endapo utaratibu wa kuziwasilisha kwa Katibu wa Bunge hatua ya kuhaririwa kwanza kabla ya kusomwa bungeni itaendelea.
Pamoja na hayo, wamesema hawatatusa bunge kwa ajili hiyo wala sababu nyingine yoyote.
Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema hayo jana Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mustakabali wa wabunge hao kuhudhuria vikao vya bunge na kuhusu kukataliwa kusomwa kwa hotuba yao bungeni jana.
Mbowe alisema anamshangaa Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kukataa kutosomwa kwa taarifa ya kambi hiyo bungeni jana kwa sababu tu haikuwasilishwa kwa Spika siku moja kabla ya kusomwa bungeni.
“Naibu Spika anasema hotuba ya KUB haipo wakati anajua kambi ilikuwa ina watumishi wanne ambao walikuwa wanafanya utafiti, kuandaa randama ya serikali, kuandaa hotuba zote zikiwamo za serikali sasa watumishi hao tangu Desemba mikataba yao iliisha na niliandika dokezo kuomba wapewe mkataba upya hadi sasa Katibu wa Bunge amekataa kufanya hivyo akidai Spika wa Bunge yuko nje kwa matibabu.
“Sawa walitaka hotuba hiyo niiandikie Segerea, kwa sababu wale vijana ndiyo walikuwa wakifanya hayo na bunge lina watumishi wa mikataba 30 wakiwamo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wote wana mikataba ya miaka miwili miwili lakini wengie wako ofisini isipokuwa wa kambi ya upinzani ambao walikufukuzwa kama mbwa katika bunge la Januari,” alisema Mbowe.
Pamoja na mambo mengine, Mbowe amesema hapatakuwa na hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni hadi watumishi warejeshwe lakini pia hata watakaporejeshwa, hawatakuwa tayari kupeleka hotuba zao kwa katibu wa Bunge akachague ni nini cha kusoma bungeni na nini cha kuacha na kwamba Bunge liking’ang’ania kufanya hivyo, hawatasoma hotuba hizo.
Akizungumzia suala hilo, Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai alisema bunge lina watumishi wa kutosha kuhudumia wabunge na ofisi zao.
Alisema hadhani kama aliyozungumza Mbowe yatakuwa na ukweli wowote kwa sababu bunge linahudumiwa na Sekretarieti ya Bunge na watumishi wake walioajiriwa na kuhudumia wabunge.
“Hatujakosa sekretarieti, nina watumishi wa kutosha kuhudumia wabunge.Kulikuwa na watumishi wa mkataba ambao mkataba wao ulimalizika Desemba, sasa alitakiwa kusema kama anawahitaji hao lakini mwenye uwezo wa kusema waendelee au wasiendelee ni Tume ya Utumishi wa Bunge.
“Kwangu alikuja akaniambia lakini sasa mimi ni mtumishi wa Bunge na kama unavyofahamu Spika wa Bunge alikuwa nje kwa matibabu.
“Watumishi walioajiriwa na Bunge wapo, mimi nikiwa mmojawapo kama mbunge anawahitaji anapewa lakini si kwa kazi binafsi. Kama anataka watumishi wa bunge kumhudumia yeye peke yake hiyo ni juu yake, wanaweza kuwa hawataki lakini sisi hatuwezi kuwalazimisha,” amesema Kagaigai.
Hovyo kabisa. Mbowe atoa msimamo mkali? Msimamo gani mkali? Siasa za hovyo kabisa anazoziendeleza Mbowe. Ni ujinga na ukosefu wa mitizamo chanya kwa upizani kufikiri kuwa ili uwe mwanasiasa mzuri ni lazima uwe mpingaji wa kila kitu. Nelson Mandela alifungwa karibu miaka 30 thelathini na makaburu. Si kufungwa tu bali watu wake waliteswa na kunyanyaswa na kuuwawa na wageni kwenye aradhi yao na Mandela alipotoka gerezani alitoka na machungu na maumivu tena makubwa. Kwani nusu ya uhai wake ulikuwa umekufa akiwa gerezani. Katika kipindi cha miaka ishirini tu 20 mwanadamu anazaa mtoto na kubadalisha taswiraya maisha ya mtu. lakini Mandela alikaa jela zaidi ya miaka ishirini na kiuhalisia hakuwa ana kosa la kukaa huko jela kipindi chote hicho. lakini alopotoka jela,Mandela alikuwa mwanadiplomasia mpole kimtizamo wa nje lakini bila ya shaka yeyote alikuwa na hasira na machungu ndani ya moyo wake na hapana shaka yeyote kilichompelekea Mandela kutoanzisha siasa za chuki zidi ya waliomsweka jela ni uzalendo wa nchi yake. Mandela hakutaka kuona South Africa being destroyed because of him, hakutaka kuona nchi yake ikikatika vipande vipande kwa maslahi ya kisiasa au umimi licha ya yakuwa chama chake ndio watu wa South Africa waliowengi. Tofauti na hawa wanasiasa wetu upinzani hapa Tanzania wanaohangaika kila kona ya dunia sijui EU,Mara Marekani,Canada na hata kuhangaika usiku na mchana kuwashawishi watanzania wawe wahasi na nchi yao, kwa lipi hasa walilofanyiwa baya hadi kuendelza siasa za hovyo zenye nia ya kuliangamiza taifa? La kushangaza zaidi harakati zote hizo za kipuuzi za akina Mbowe zinaelekezwa kwa kiongozi amabae amejiapiza kupambana katika kuhakikisha Tanzania na watanzania wanaondakana na unyonge wa maisha. Si hilo tu Magufuli na chama ndio watanzania waliowengi hata wawakishi wa wananchi bungeni CCM imewazidi wapinzani kwa mbali kabisa. Sasa katika hali hii ya siasa za kipumbavu za akina Mbowe na wenzake watanzania tuna kila sababu ya kuwaita kuwa ni maadui wa nchi. Ni watu wa hovyo ni aibu hata kuwaita wanasiasa kwani neno siasa halina maana ya uadui.kunapotokea mtafaruku baina ya watu jamii hukimbilia kwa wanasiasa kuleta maelewano,sasa wanasiasa wetu wa upinzani ni watu wa kutafuta mtafaruku katika jamii zetu sasa hapo utaona lazima watanzania tusiwe mabwege kuwachekea hawa watu madhara yake ni makubwa.
ReplyDelete