Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Viongozi wenzake watano tayari wameshafikishwa mahakama ya kisutu ni tangu saa mbili asubuhi hii na sasa wanasubiri shughuli za kimahakama zianze ili wakamilishe masharti ya dhamana.
Mbali ya Mbowe wengine ni Katibu Mkuu Dk Vicent Mashinji, Manaibu Katibu wakuu John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu (Zanzibar), Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake wa chama hicho Ester Matiku wanakabiliwa na kesi ya jinai, wakidaiwa pamoja na mambo mengine ikiwamo kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali.
Wamekuwa mahabusu tangu walipopandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo March 27, 2018.
Mbowe na Vigogo Watano Chadema Wafikishwa Mahakamani Kukamilisha Mashariti ya Dhamana
1
April 03, 2018
Tags
Hawa akina Mbowe zamana ya nini? Sheria inaeleza wazi kabisa ukifanya maandamano au mkusanyiko haramu wa kuipinga serikali ni uhaini. Lakini mbaya zaidi katika maandamano yale haramu ya akina Mbowe yalisababisha upotevu wa mali na maisha ya watu sasa kwa kweli hapo hatuhitaji siasa katika kusimamia sheria hahihalisi mwanasiasa mkubwa au mdogo watanzania tunataka kuona hawa watu wanachukuliwa hatua kwa kuvuruga amani ya nchi.
ReplyDelete