Mbunge Aukosoa Wimbo wa Taifa

Mbunge Aukosoa Wimbo wa Taifa
Mbunge wa Mbinga mjini, Sixtus Mapunda amedai bungeni kuwa, wimbo wa Taifa unaoimbwa bungeni si rasmi na amehoji kama ni sahihi kuendelea kuutumia.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo, alieleza kuwa huo unaotumika bungeni una makosa matatu yakiwemo ya maneno, ala na midundo.

Ameyasema hayo kwenye kikao cha kwanza cha Mkutano wa 11 wa Bunge wakati anaomba mwongozo wa Spika baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Kwa mujibu wa Mh.Mapunda, wimbo wa taifa unaotumika bungeni ni tofauti na ulioidhinishwa na lililokuwa Baraza la Muziki Tanzania (BAMUTA) na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema, kabla ya kutoa mwongozo alisema ni lazima ajiridhishe kwa kuusikiliza kwanza“Kwa hiyo kama kutakuwa na makosa nitatoa mwongozo hapo baadaye.” alisema Dk. Ackson.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad