Mbunge Selasini Aibana Serikali Kuhusu Viti Bungeni "Kiti Nilichokalia Kimenifinya Makalio"

Mbunge Selasini Aibana Serikali Kuhusu Viti Bungeni "Kiti Nilichokalia Kimenifinya Makalio"
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) ameomba mwongozo bungeni akitaka viti vya bungeni kukarabatiwa kwa kuwa viti hivyo ni vibovu.

“Ni lini serikali itakarabati viti hivi, hiki nilichokalia leo asubuhi kimenifinya makalio,“ alihoji.

Salasini ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma, wakati wa kipindi cha Maswali na majibu huku akiitaka serikali itoe majibu ni lini viti hivyo vitakarabatiwa.

Aidha Mbunge huyo amesema kuwa kiti hicho alichokalia leo katika bunge hilo kimemfinya makalio. Sambamba na kuomba muongozo huo Spika Ngudai amesema kuwa suala hilo limepokea na litatolewa ufafanuzi.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad