Kisa kimoja kimezua hisia huko nchini Australia baada ya mbwa mmoja mzee aitwaje Max kukaa na kumlinda mtoto mdogo ambaye alipotea kutoka nyumbani kwao kwa saa 15.
Inaelezwa kuwa mtoto huyo aliondoka akiwa anacheza tu na kutoweka kwa saa 15 huku akizua taharuki kwa ndugu na watu mbalimbali kumtafuta na baadaye kumpata porini akiwa na mbwa huyo Max.
Kwa saa zote hizo mtoto huyo wa miaka mitatu anayejulikana kwa jina la Aurora alikuwa na mbwa katika vichaka vya eneo la Queensland’s Southern Downs.
Baada ya kumpata mtoto polisi waliokuwa kwenye msako na ndugu, walimpa mbwa huyo heshima ya kuwa ”mbwa wa polisi wa heshima’ kwa kumlinda mtoto huyo.