Mwanzoni mwa wiki hii wazazi waliyoachiwa watoto na wenzao bila kupata huduma za kimalezi walifika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kwa ajili ya kupata msaada wa kisheria. Katika wale waliyoenda mama aliyeonekana akiwa na mtoto mwenye asili ya China aligonga vichwa vya habari vilivyo.
Hapo baadaye ilikuja kufamika ni kweli mama huyo aliolewa na raia wa China na kujaliwa kupata mtoto ila kwa sasa mzazi mwenzie hayupo tena nchini kwani amesharejea kwao na hatuoi matunzo ya mtoto.
Sasa leo, April 14, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amesema raia huyo wa China anafuatiliwa kupitia ubalozi na kuna matumaini ya kupatikana.
“Nimeongea na ubalozi wa China tayari tumeshawapa maelezo na wameamua kuyatuma nchini kwao kwenye ile kampuni aliyokuwepo, kwa hiyo tunafuata process zote,” amesema RC Makonda.
“Na kwa mazungumzo tuliyokuwa nayo kwa awali kutoka ubalozi wa China wanakubali kwamba endapo mtoto yule ikibainika atakuwa na wajibu wa kumtunza, kwa hiyo muda si mrefu maisha ya yule mtoto yanaweza yakabadilika, akapata neema ,” amesema.
RC Makonda ameongeza kuwa zoezi hilo halitaishia kuwasaka wale waliowatelekeza watoto na wapo nje ya mkoa wake, bali hata walio nje ya nchi kupitia balozi za Tanzania kwani zinasaidia