Miili ya wanajeshi nane wa Uganda waliouawa katika shambulio lilitekelezwa na kundi la Al shabaab imerejeshwa nyumbani na kukabidhiwa familia zao kwa maziko.
Kwa mjibu wa msemaji wa jeshi la UPDF idadi wanajeshi wa Uganda waliouawa imeongeza hadi nane, baada ya wajeruhiwa wanne kufariki.
Jeshi la Uganda linasema zaidi ya wapiganaji 30 wa Al shabaab waliuawa katika shambulio la Jumapili.
Mwandishi wa BBC, Isaac Mumena anaelezea kuwa bendi ya jeshi la UPDF walipokea miili ya wanajeshi wa Uganda katika uwanja wa kijeshi wa Entebbe.
Naibu wa Kamanda wa majeshi ya nchi kavu Meja Jenerali Sam Kavuma ndiye aliyepokea miili ya wanajeshi wanne waliofikishwa Jumanne kuwapongeza marehemu hao kwa kazi waliofanya.
Kamanda Kavuma alisema "hawakufa bure, wamefanya kazi nzuri. Wapewe pongezi,waliweza kuwazuia wanamgambo wa Al shaabab wasifanye mashambulizi yao na kuwaangamiza."
Miili ya wanajeshi wanne walioletwa ni wale waliofariki papo hapo kwenye mapambano na kati ya majeruhi sita, wanne walifariki wakiwa hospitali na kuhitimisha idadi ya wanajeshi nane.
Kikosi cha wanajeshi kutoka Uganda wakipiga doria kwenye mji wa Afgoye kusini mwa Mogadishu mwaka 2014Haki miliki ya pichaAFP
Image caption
Kikosi cha wanajeshi kutoka Uganda wakipiga doria kwenye mji wa Afgoye kusini mwa Mogadishu mwaka 2014
Naibu wa msemaji wa jeshi la UPDF Luteni Kanali Deo Akii siku ya Jumatatu alifahamisha BBC kwamba wanamugambo walishababu zaidi ya 30 waliuwa.
" Wanamgambo 30 wa Alshababu waliuwawa kwa upande wetu kwa mapingano hayo tumepoteza wanajeshi wanne na saba kujeruiwa." alisema
"Mapigano hayo yamekuwa katika eneo la 'sekta one' , ambayo 'sekta one' ni eneo la wanajeshi wa Uganda, ni eneo ambalo Al shabaab wanapenda kulichukuwa, ni sehemu muhimu kwa serikali ya Somalia."
Licha ya maafa hayo ya wanajeshi wa Uganda kutokea, jeshi la Uganda limeapa kuendelea na juhudi zake za kulinda amani nchini Somalia chini ya kikosi cha AMISOM.
Pamoja na hayo wameahidi kuwasaka wanamgambo wa Al shabaab nchini Somalia hadi watakapowamaliza na wananchi wa Somalia kuishi kwa amani.
Julai 2016, Umoja wa Afrika ulitangaza mipango ya kuwatoa kwa awamu wanajeshi nchini Somalia, kuanzia Oktoba 2018 na kumalizia mpango huo mwishoni mwa waka 2020.