Mbunge wa Jimbo la Geita vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) ameuponda utaratibu wa serikali kufungia nyimbo za wasanii pindi zinapoonekana kukiuka maadili.
Akizungumza leo Bungeni April 27, 2018 wakati akichangia bajeti ya wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaaa na Michezo, Musukuma amesema serikali inatakiwa kutoa elimu zaidi kuliko kufungia.
“Msitumie muda mwingi kufungia, ni bora ukatumia muda mwingi kuwafundisha na kukemea yale mambo madogo madogo ili hii tasnia iendelee,” amesema.
“Mnamsumbua Diamond hapa masikini ya Mungu, mnaona yaliyofanyika Kenya, wenzenu wamempokea wanamuambia imba kila kitu ambacho umezuiliwa, wamempa kiwanja, wamempangia nyumba, tutapoteza hizi bahati,” amesisitiza.
Utakumbuka February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari.
SOMA Pia: Job Opportunity at Uchumi Commercial Bank Ltd, Head of Internal Audit
Mnamsumbua Diamond Hapa, Kenya Wamempokea na Nyumba Wamempangia – Musukuma
April 28, 2018
Tags