Monalisa alisindikizwa na mama yake mzazi katika makabidhiano hayo katika ofisi za BASATA na makabidhiano hayo yalihudhuria na watu mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe pamoja na Katibu mtendaji wa BASATA Godfrey Mwingereza.
Monalisa ametoa shukrani zake za dhati kwa Watanzania wote waliompigia kura na kusema kuwa hata asiporudi na ushindi lakini ana amini kuwa haiwezi kukosekana tuzo ya Ray Kigosi, Mzee Majuto au Moiz Hussein na kuahidi kutuwakilisha Watanzania vizuri kwa kuipeperusha bendera ya Taifa.