Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, umesimamishwa na wananchi wa eneo la Migori mkoani Iringa ili kutoa kero zao zinazowakabili, kwa kiongozi huyo mkubwa wa nchi.
Msafara huo ambao ulikuwa ukipita kuelekea mkoani Irnga kwa ajili ya tukio la uzinduzi wa barabara ya Iringa Migori yenye urefu wa km 189, umelalamikiwa kero mbali mbali zinazowakabili wananchi wa eneo hilo pamoja na changamoto zinazoikabili shule ya sekondari Nyerere iliyopo mkoani Iringa, na kutoa fedha taslim shilingi milioni 5 ili kusaidia ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu.
Baada ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Walend Manga kuelezea hatua walizofikia za ujenzi wa nyumba za walimu wanazojenga kwa nguvu yao na wananchi, pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kwa fedha zinazopelekwa mashuleni, Rais Magufuli alisikika akisema ..."Ahsante sana Mwalimu Mkuu, shule yenu ina jina zuri, jina la Nyerere, na mimi nitawaongezea milioni 5, sina milioni tano hapa!!? Hebu nisaidie hapa hapa kabisa, bahati nzuri nina milioni 5 hapa, nakupa hapa hapa, kazitumie vizuri, mimi huwa nafuatilia, siku moja nitapita hapa nicheki hizi milioni tano zimetumika wapi.
Sambamba na hilo Rais Magufuli amemtaka Mkandarasi aliyepewa jukumu la kusambaza miundombinu ya umeme kwenyye eneo hilo kukamilisha mapema, ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha, Rais Magufuli amewataka wanakijiji hao kuchapa kazi na kutumia barabara ya lami ya Iringa-Dodoma kujitajirisha.
“Barabara imekamilika mnaiona, itumieni ili mtajirike, limeni mazao kwa bidii na msafirishe kwenda sehemu mbalimbali za nchi,” amesema Rais Magufuli.
Aliwataka kutumia mvua zinazoendelea, kulima na kufuga ili waweze kunufaika.