Msichana Aibukia Kwa RC Makonda na Kudai Ametelekezwa na Baba yake Ambaye ni Mzee Edward Lowassa

Mdada mmoja ameitikia wito wa Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda kuhusu wanawake waliotelekezewa watoto kufika ofisini kwake ili kupata msaada wa kisheria. Dada huyo amejitokeza na kudai yeye ni mtoto wa Mzee Edward Lowassa.

Amesema..
''Nimetokea Kigamboni, nimekuja hapa, nimekuja kusikiliza wito wa mkuu wa mkoa, Makonda kwamba watu ambao wametelekezwa. Sasa mimi ni mmoja wa mtoto ambaye niliyetelekezwa, ambaye baba yangu ni Edward Lowassa. Nimeanza kumtafuta toka nikiwa darasa la sita na mama ananambia ni kweli baba yako ndio huyo huyo. Sasa nimefuatilia kila sehemu lakini sioni mafanikio kwa hiyo nimekuja hapa kwa mkuu wa mkoa Makonda anisaidie kwa hali na mali kwa vyovyote vile itakavyokuwa kama nipo tayari nipimwe DNA na huyo mzee Lowassa ili nisaidiwe nijue nakaa wapi. Kwasababu mama yangu mzazi yupo hata akija atatoa ushahidi na atasema kwamba itakuwaje kama DNA nipimwe basi.''​

VIDEO:
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad