Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amejibu tuhuma za
kutelekeza mtoto, baada ya picha kuzagaa kwenye mitandao ikimuonyesha
mtoto ambaye amefanana naye akitajwa kumtelekeza.
Akizungumza na
www.eatv.tv,
Peter Msigwa amesema kwamba alichokiandika kwenye mitandao ya kijamii
anamaanisha hivyo anamtaka mwanamke huyo ambaye ametajwa kuwa miongoni
mwa walioenda kwa mkuu wa mkoa wa Dar e salaam Paul Makonda kwa
kutelekezwa, asiishie hapo tu bali aende hata Bungeni.
“Ilikoanzia imeanzia kwa Jerry Muro ndiye kasambaza hizi habari, kitu
ambacho nakijibu hapa amekianzisha Jerry Muro, sasa mimi nasema kama
huyo mtu yupo, nimetoa namba zangu na kama sipatikani aje hapa Bungeni”,
amesema Peter Msigwa.
Hapo jana Peter Msigwa ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa
facebook akisema kwamba iwapo kweli mwanamke huyo yupo na akithibitisha
ni kweli amemtelekeza, basi yupo tayari kujiuzulu ubunge wake alionao.
Ujiuzulu ubunge ili iweje. acha ujinga bhana mwambie aje tuu tutamhudumia
ReplyDeleteKm ikithibitika, badala ya kuresign, si ndo umhudumie mwanao, na ubunge utakusaidia kuongeza uwezo kifedha ili kutoa huduma bora kwa mwanao. Hakuna binadamu aziyekosa
ReplyDelete