Mtangazaji wa Cloud Michael Lukindo aacha kazi ya utangazaji,aamua kufanya muziki...Afuata nyazo za kina Ray C

Kama wewe ni msikilizaji mzuri wa radio hasa Cloud Fm basi utakuwa unamfahamu au kuwahi kumsikia mtangazaji Michael Lukindo.
Habari ni kwamba Michael Lukindo ameamua kuachana na mambo ya utangazaji na kujikita katika masuala ya muziki kwa sababu ameona ana kipaji kizuri cha kuimba.

Michael lukindo ambae alifaamika kwa jina la Mr Infoma aliacha kusikika Cloud Fm tangu mwezi februari mwaka huu.

Maamuzi ya namna kama hiyo yamewahi kufanywa na wasanii Ray C na Vanessa mdee mabao waliacha kazi ya utangazaji na kuamua kujikita kwenye Muziki.

Kwa sasa Michael Lukindo anatamba na wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni unaoitwa "Basi iwe",unaweza kuupata kwenye YouTube channel yake ya Michael Lukindo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad