Muhubiri Dar afunguka kutoza malipo kwa kila anaetaka kuombewa na yeye

Prophet Nicolaus Suguye wa Kanisa la WRM Kivule Dar es salaam amefunguka kuhusu taarifa za yeye kulazimisha kila Mtu anaetaka kuombewa na yeye kulipia maombezi hayo kwa lazima kanisani kwake Kivule Dar es salaam.

Phrophet Suguye ameongea na millardayo.com na AyoTV na kusema kilichotokea ni kwamba aliomba Watu wanaokwenda kuombewa nae kuchangia pesa kwa ajili ya kuanzisha TV ya kanisa iitwayo WRM ambayo inapatikana STARTIMES na kwenye AzamTV, hivyo hakulazimisha.

“Nilisema wale wanaotaka kuja kuombewa kwenye ibada kanisani iliku bure kabisa lakini kwa waliotaka kuniona wenyewe ofisini kwangu ndio nilisema wachangie TV, hata hivyo hakuna tena huo utaratibu wa kuchangia TV, hiyo laana ya kutoza watu pesa kwa maombezi sina” – Nicolaus Suguye
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Km ni mtumishi wa Bwana Yesu, bado hata watu kuja kukuona ofisini kwako au kokote, usingeoaswa ku associate hizo meetings na pesa, hata Kama ni za kuchangia TV. Na swali kwa mliompa pesa ili kumuona, kwanini mlifanya hivyo? Siku nyingine mtu akikuomba pesa msaidie kwa kumuuliza kama je anaruhusiwa kuchukua pesa?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad