Muimbaji Ray C amefunguka mazito kwa kile anachoona kinaenda ndivyo sivyo katika muziki wa Bongo Flava kwa sasa.
Ray C amefikia hata hatua ya kutumia maneno makali kueleza hisia zake kwa yale ambavyo hakubaliani nayo kwenye tasnia hiyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
Kuna muda huwa nafikiria mambo mengi sana! kuna muda najiskia kuamua kutiwa mimba, nizae niwe tu mama wa nyumbani! maana kuna muda nikiangalia wasanii wenye maendeleo kwenye Bongo Flava ni wachache saaaaana! na sijiongelei mimi maana mimi mwenyewe kuna wakati nilivurunda mwenyewe!
Nakubali nilibugi na nikagundua nimebugi haswa na ndio maana nimepambana mpaka hapa niliko baada ya kugundua baraka tele nilizozawadiwa na Mungu ni kubwa mno kuliko starehe za muda za ndogo na za kibwege!!! Ila huwa nakaa najiuliza miaka kama sita ambayo nilipotea kwenye industry! kuna wasanii nilianza nao na wana vipaji vya ajabu maskini lakini wengi wao wamezimwa kama taa!!!
Namkumbuka Nature, Joseline, Bushoke, Z Anto, Matonya, Makamua, Marlow, Domokaya n.k😢 majina ni mengi siwezi maliza!!!!!Wengi sana ni wasanii wakubwa sana na wana uwezo mkubwa mno. Najiuliza kitu gani kinachowakatisha tamaa hadi leo wamekuwa hadimu!!!???Mi nilikuwa kimya kutokana na sehemu.niliyokuwepo!!NAMAANISHA!? Jehanam!! na hawa niliowaacha je??? Kuna nini kwenye bongo flava???
Wasanii wapya ni wengi yes nalijua hilo lakini ukweli ni kuwa nchi yoyote hapa Afrika Mashariki nikienda naskia tu nyimbo za zamani nyingi na mpya pia!! mimi mwenyewe pamoja na mahanjumat ya pepo ya ahera yote lakini bado sauti ipo na nyie je???Nahisi kuna jini mmoja kwenye hii industry anaesababisha wasanii wengi wajione kama ndo basi tena! point yake ni moja! Na uwezo wa kukujenga na kukumaliza mara moja!!!maana yake nini sasa???.
Mungu anisamehe nianze kwenda kabla ya huyu jini!Pesa!! pesa!Pesa!Pesa!Ingekuwa pesa ndo uhai wallah hata Michael Jaclson asingekufa!!!!.
Nimeitumia hiyo picha sababu roho imeniuma siku ya mwisho kabisa ndo venue inabadilishwa!!!!Kuna karoho tu kamenikasirisha nimehisi kama kuna upuuzi wa kisengwile umefanywa ili mradi tu waharibu shughuli ya dada wa watu! Roho ya ndani huongea ukweli na ndo ninachohisi siku ya leo.
Wasanii mna kazi kubwa ya kuanza kujiamini kwanza kabla ya kuamini mtu mwingine! Mkishajua aliewapa vipaji naamini Mtasimama tena, Mtaingia studio tena! Maana mashabiki wenu bado wapo!!! Kinachohitajika ni kipaji sio promota anaefikiria tumbo lake na mpaka leo anazidi kukondeana!! ziba lakini tutakutana kaburini!.