Mwenyekiti Apotea Kigoma Zitto Kabwe Awasha Moto Bungeni

Mwenyekiti Apotea Kigoma Zitto Kabwe Awasha Moto Bungeni
MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT -Wazalendo), Zitto Kabwe amemtaka Waziri wa Ofisi ya Rais -Tamisemi kulitafutia ufumbuzi suala la kutoweka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kakonko mkoani humo, Simon Kanguye.
Zitto amefunguka hayo jana Aprili 12, 2018 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais, yenye Wizara za Tamisemi na Utumishi na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
“Habari zinazosambaa Kibondo tayari ameuawa. Tunataka maelezo ya mtu huyo, sisi watu wa Kigoma ni Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania naomba hilo mlielewe,” alisema Zitto.
Zitto alisema kiongozi huyo hajaonekana kwa miezi tisa sasa ambapo mara ya mwisho kuonekana aliitwa kwa mkurugenzi na kukutana na Ofisa Usalama wa Wilaya ambao amedai tangu siku hiyo hajulikani alipo mwenyekiti huyo licha ya jitihada za ndugu na viongozi wenzake kumtafuta bila mafanikio.
“Familia imechukua hatua mbalimbali, imelalamika na sisi wajumbe wenzake tumehoji kwenye vikao, hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini, kamwe hatutokubali,” alisema Zitto.

SOMA PIA: Job Opportunity at eWallet Africa Ltd, Sales and Marketing Manager

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad