Mzee Majuto Azidiwa Tena Na Kurejeshwa Kulazwa Hospitalin

Dar es Salaam. Muigizaji na mchekeshaji wa siku nyingi, Amri Athuman maarufu Mzee Majuto, amelazwa tena katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam, baada ya kuzidiwa.

Mke wa mwigizaji huyo, Aisha Yusufu, ameiambia MCL Digital leo Aprili 23 kwamba mume wake walimpeleka hospitalini hapo leo saa 7:00 mchana.

Aisha amesema kidonda alichofanyiwa upasuaji kimeleta shida, hivyo kumpeleka kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Majuto alilazwa hospitalini hapo Januari mwaka huu na kufanyiwa upasuaji wa tezi dume.

Source: Mwananchi
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MCHANGIENI MATIBABU.MUSINGOJE AONDOKE DUNIANI NDIO MUCHANGE PESA ZA MAZISHI.KUWENI WATU WAIMANI.LEAVE IN PEACE BEFORE REST IN PEACE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad