Ndoa ya Alikiba Yapanda Moto Ndugu na Rafiki wa Karibu Waanza Kutua Mombasa

Ndoa ya Alikiba Yapanda Moto Ndugu na Rafiki wa Karibu Waanza Kutua Mombasa
Ujio wa ndoa ya Alikiba kwa sasa ndio imeteka vichwa vya habari mjini.



Tayari maandalizi muhimu yameonekana kuanza kukamilika huku watu wa karibu wa msanii huyo wameonekana kuanza kutua mjini Mombasa, Kenya kwa ajili ya kuhudhuria ndoa hiyo.



Baadhi ya picha tayari zimeanza kusambaa mitandaoni zikiwaonyesha watu hao akiwemo msanii wa filamu Bongo, Esha Buheti na dada yake Alikiba, Zabibu na wengine.



Wakati huo huo Abdu Kiba ameweka moja ya picha hizo kwenye mtandao wa Instagram na kuandika ujumbe unaosomeka, “MY TEAM 💣💣💣💣 Mombasa kitaelewekaa tu.”

Alikiba anatarajiwa kufunga ndoa na mrembo Aminah Rikesh April 26, 2018 katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo mjini Mombasa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad