Ndugai Aungana na Mbunge CCM

Ndugai Aungana na Mbunge CCM
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewashauri Wabunge wanawake kuungana na kupeleka hoja ya kuwasaidia kina mama wanaoteseka magereza kwa kufungwa kwa madeni madogo madogo huku wakiwa na watoto na wenye maradhi ambao serikali inapaswa kuwagharamia kila siku


Spika Ndugai ametoa ushauri huo baada ya Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko kuhoji, kwanini serikali isitumie busara zaidi kwa wafungwa hususani wakina mama wenye watoto wachanga ambao wanafungwa kwa kesi za kudaiwa laki 1-2 halafu wanafungwa miezi 6 kwa maana wanakuwa wanaenda kutumia gharama kubwa kuliko deni wanalodaiwa.

Hata hivyo swali la Esther Matiko lilijibiwa na William Tate Ole -Nasha amesema suala hilo ni la kisheria hivy kama Mbunge huyo ameona sheria hiyo imepitwa na wakati na haitendi haki anapaswa kupeleka hoja ya sheria bungeni ili iweze kubadilishwa.

Naye Spika Ndugai ameongeza "Na kwa kweli wabunge wanawake mpo wengi hapa kama mambo hayo yapo kweli mnapaswa kuungani ili kuangalia mateso ya kina mama wa aina hiyo".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad