Ndugai Leo Amerejea Bungeni kwa Kishindo

Ndugai Leo Amerejea Bungeni kwa Kishindo

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, leo amerejea Bungeni na kuendesha kikao cha Bunge, baada ya muda mrefu wa kuwa nje ya nchi kwa matibabu.


Tukio la Ndugai kurejea Bungeni limeonekana kufurahiwa na baadhi ya wabunge huku wakielezea hisia zao, na kumshukuru Mungu kwa kuweza kuungana nao tena.

“Tunafurahi kuona umerejea na kuungana nasi tena, baada ya kukumisi kwa muda mrefu, na sisi tuko salama tangu ulivyotuacha”, alisikikia Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe akimueleza Spika Ndugai aliposimama kujibu swali la mbunge, kitendo ambacho kimejirudia mara kwa mara kwa wabunge wengine.

Job Ndugai alikuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miezi miwili akiwa kwenye matibabu, huku kukiwa na tetesi kuwa alikuwa akiumwa sana, lakini amerejea hivi karibuni akiwa na afya njema na kuendelea na majukumu yake ya Bunge.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad