Hapo jana Real Madrid wameendeleza rekodi yao nzuri katika michuano ya Champions League baada ya kuichapa Bayern Munich kwa mabao 2-1 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufudhu fainali za Champions League.
Joshua Kimmich aliifungia Bayern Munich bao la kuongoza, bao la Kimmich lilikuwa bao la 100 kwa kocha Jupp Heynckes katika michuano ya Champions League.
Marcelo aliisawazishia Real Madrid,hili lilikuwa bao lake la 3 msimu huu na hii ikiwa msimu wake aliofunga mabao mengi katika Champions League, Marco Asensio bao lake la ushindi lilikuwa bao lake la 3 kama sub msimu huu.
Ushindi wa mabao ya jana kwa Real Madrid umewafanya kushinda michezo 150 katika Champions League, na sasa wanakuwa timu ya kwanza kushinda idadi hiyo ya michezo katika ligi hiyo.
Sii hivyo tu bali pia ushindi wa jana wa Real Madrid unamfanya Cristiano Ronaldo kuvunja rekodi ya Iker Casillas ya ushindi wa mechi 95 katika Champions League na sasa CR7 anakuwa ameshinda mechi 96, japokuwa jana ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa Cr7 kutofunga katika mechi 12 za CL.