Prof Tibaijuka- Hata Sisi Tuliosingiziwa Kuna Siku Watakuja Kujua Ukweli

Prof Tibaijuka- Hata Sisi Tuliosingiziwa Kuna Siku Watakuja Kujua Ukweli
Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu kufariki kwa aliyewahi kuwa mke wa Raisi wa kwanza wa Afrika Kusini Winnie Mandela, Mbunge wa Muleba kusini Prof Anna Tibaijuka  ameonesha kukerwa na baadhi baadhi na tuhuma alizowahi kupewa mwanaharakati huyo ikiwemo kuua.

“Sasa hivi Winnie Mandela ndio anatambuliwa kwamba aliweka mchango mkubwa, kwanini wakati wa uhai wake alifanyiwa kila hila na kusingiziwa? Mimi kusingiziwa nakujua…! wanasema aisifiaye mvua imemnyea”

“Winnie Mandela alisingiziwa mambo makubwa kwamba aliua mototo lakini leo wanasema ilikuwa dili tu kumchafua Yule mama. Hii inatupa moyo hata sisi ambao tumesingiziwa mambo kwamba kuna siku watu watakuja kujua ukweli uko wapi na watabaki kushangaa ” –Prof Anna Tibaijuka

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad