Rais Magufuli Atajwa Kuwania Tuzo Afrika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, zijulikanazo kwa jina la The African Prestigious Awards zinazotarajia kufanyika nchini Ghana.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dk. Harrison Mwakyembe wakati akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana katika tuzo hizo ambapo ameweka wazi kwamba Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika.

Amesema kuwa Utendaji uliotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na ukuwaji wa sekta ya filamu nchini ndiyo vinavochangia kuitangaza nchi yetu katika tuzo za The African Prestious Awards.

“Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, napia tuna wasanii watatu ndani ya tansia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika"  Dkt.Mwakyembe.

Ameongeza "Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora Afrika".

Monalisa anatarajia kuondoka nchini mapema wiki hii kwenda nchini Ghana kwa ajili ya Tuzo hizo ambapo amewaahidi watanzania kuwa lazima atarudi na tuzo kwani anawawakilisha wasanii wenzake hao wawili pamoja na mpiga picha huyo aliyetajwa na pia aliishukuru serikali kwa kumpatia tiketi kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad