Rais wa Zamani wa Brazil Ajisalimisha Gerezani Kutumikia Kifungo cha Miaka 12

Rais wa Zamani wa Brazil Ajisalimisha Gerezani Kutumikia Kifungo cha Miaka 12Leo April 9, 2018 stori ninayokusogezea ni kuhusu Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva amejisalimisha katika gereza la Curitiba tayari kuanza kutumikia kifungo cha miaka 12 baada ya awali kukwepa kufanya hivyo.

Ijumaa Mahakama ilimhukumu kwa mashtaka ya ufisadi, lakini alikimbilia katika makao makuu ya muungano wa wafanyakazi mjini Sao Paolo, ambako wafuasi wake walitaka asijisalimishe.

Televisheni nyingi nchini Brazil zimeonesha alivyowasili kwa helikopta katika Makao Makuu ya Polisi katika mji wa Curibita.

Lula alitoa hotuba katika mji wa Sao Bernardo do Campo kabla ya kujisalimisha, Lula amejitaja kuwa raia aliyekasirishwa na mashtaka ya kutungwa ya ufisadi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad