Romy Jons ambaye ni Dj wa Diamond Platnumz amemuomba msamaha Barakah The Prince na mpenzi wake Naj kwa yale yaliyojitokeza siku chache zilizopita.
Romj alituhumiwa kumtongoza Naj kupitia DM ya Instagram huku akionekana kumkashfu Barakah wakati akimpa maneno matamu mrembo huyo.
DJ huyo ameowaomba radhi wawili hao kupitia mtandao wa Instagram kwa kuandika:
NICHUKUE FURSA HII KUMUOMBA RADHI MSHKAJI,RAFIKI,NDUGU YEYE PAMOJA NA MPENZI WAKE KAMA NIMEWAKWAZA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE,NISINGEPENDA HAYA MALUMBANO YAENDELEE KWA SISI KAMA VIJANA INATUPASA TUKAE TUPANGE TUNAWEZAJE KUJIKWAMUA NA HUU UMASIKINI NA SANAA YETU KWA UJUMLA!!!!PIA NIOMBE RADHI KWA FAMILIA YANGU,NDUGU ZANGU,MARAFIKI ZANGU NA MASHABIKI ZANGU KWA UJUMLA KWA LOLOTE LILILOJITOKEZA!!! MUNGU ATUONDOLEE UADUI NA TUENDELEE KUFANYA KAZI INSHAALLAH
Siku ya jana pia Romy alimuomba msamaha mkewe kutokana na tukio hilo ambalo lilionekana kuelekea kuvunja ndoa yake.