Rostam Wapo Katika Hatua za Mwisho Kukamilisha Video Yao na Khaligraph Jones

Rostam Wapo Katika Hatua za Mwisho Kukamilisha Video Yao na Khaligraph Jones
Roma na Stamina ambao wanaunda kundi la Rostam wapo katika hatua za mwisho kukamilisha video ya wimbo wao waliofanya na Khaligraph Jones kutoka nchini Kenya.

Kwa sasa kundi hilo lipo nchini Kenya kwa ajili ya ku-shoot video ya wimbo wao ambao waliurekodi September mwaka jana wakati kundi hilo lilipofanya tour nchini humo

Si Rostam pekee waliofunga safari na kumfuata Khaligraph Jones kwa ajili ya video, siku chache zilizopita Young Killer alikuwa Kenya ambapo wali-shoot video yao licha ya wimbo wao kuwa tayari umevuja.

Rosta wanaungana na wasanii wengine kutoka Bongo kama Chin Bees, Rayvanny, Christian Bella, Rosa Ree na Stereo kufanya kazi na Khaligraph Jones. Pia wasanii wote wa Bongo waliowahi kufanya kolabo rapper huyo na kutoa video walimfuata Khaligraph Kenya kwa ajili ya video.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad