Mbunge wa Ulanga Gudluck Mlinga ameitaka Wizara ya Katiba na Sheria kutoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na zoezi linaloendeshwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda la kuwatambua wakina baba waliowatelekeza watoto wao.
Akitoa hoja hiyo wakati wa kuchangia Bajeti ya Waziri wa Katiba na Sheria Mlinga amesema zoezi linaoendelea jijini Dar es Salaam linadhalilisha watu na halina staha katika jamii.
Aidha, baadhi ya wabunge wakapata fursa ya kuchangia hoja ya Mlinga na kutoa tahadhari. Waziri wa katiba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakapata fursa ya kujibu hoja hizo za wabunge
.Makonda hana kosa lolote lile kama Mkuu wa mkoa akitafuta njia za kusaidia wananchi wake. Na kwa kiwamgo cha wananchi walivyojitokeza basi inaonesha dhahiri taasisi husika na masuala ya jamii hazifanyi kazi zake ipasavyo. Kama mkuu wa mkoa Makonda ana washauri na wanasheria kwa hivyo watu wasi kimbilue kumlaumu tu. Nnaimani kabisa hao wabunge wanaomnyooshea kidole makonda kuna matatizo makubwa ya wototo waliotelekezwa na wazee wao katika majimbo yao. Ingekuwa busara kwa hao wabunge wanaomlaumu Makonda kuonesha mfano Kwanza kwenye majimbo yao kiufasaha ya vipi wameyatatua matatizo ya wototo waliotelekezwa kabla ya kumnyooshea kidole Paul Makonda otherwise wao wenyewe wawe wa kuchunguzwa kwanza.
ReplyDeleteHAYO NDO NILOTAKA KUYAONGEA MM KUTOKA MOYONI MWANGU... Ingekuwa busara kwa hao wabunge wanaomlaumu Makonda kuonesha mfano Kwanza kwenye majimbo yao kiufasaha ya vipi wameyatatua matatizo ya wototo waliotelekezwa kabla ya kumnyooshea kidole Paul Makonda otherwise wao wenyewe wawe wa kuchunguzwa kwanza...BOG UP MACO..ALUNTA CONTINUA...
ReplyDeleteNi jukumu la Serikali kushughulikia watoto waliotelekezwa. Nchi zenye uwezo huingilia kati tatizo la utekelezaji wa watoto kwa kukunyang'anya watoto uliowatelekeza na kuwaweka sehemu salama na kuwapata tena inaweza kuwa taabu. Paul umefanya ubunifu mzuri. Watoto wengi kwa sasa wanaishi mitaani kisa hawakuwa na wa kuwalea. Baadaye wanakosa maadili ndipo matatizo mengine huzuka kama 'panya Road'. Binti anaweza kujikuta ameingia kwenye uchangu doa, kisha naye anazaa bila na kuwa wa kumsaidia kulea. Tatizo linakuwa halina mwisho kama vile muunganiko wa chain mwisho wa yote ni kukosa elimu kwa kutoenda shule na kisha ufukara wa kurithishana. Paul Makonda Acha kusikiliza hizo kelele,chapa kazi mheshimiwa
ReplyDelete:)
Makonda yupo sahihi, nyie mnaomlaumu na nyie inaonesha mnahusika katika kutelekeza watoto ila mna kihoro na nyie kuja kutajwa na wanawake mliowatelekeza
ReplyDelete