Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde amelieleza bunge kuhusu tuhuma za baadhi ya wabunge kuhoji uhalali wa Serikali kutumia nembo ya taifa ambayo picha zilizopo haziakisi uhalisia wa mwanamke wa kitanzania.
Mavunde amesema…>>>“Yamesemwa maneno kwamba nembo yetu haiakisi muonekano wa kitanzania kwamadai kwamba mwanamke aliyepo amevaa wigi, sio kweli kwamba haiakisi nah ii ni moja ya alama ya taifa”
Mbona hiyo Nembo ya Taifa ipo bomba tu. Picha ina ujumbe unaojieleza bila ya maandishi yakuwa Mwanamke na Mwanamme wakitanzania wapo bega kwa bega wakishiriki kulijenga Taifa lao. Picha inayowakilisha usawa katika majukumu kati ya mwanamke na Mwanamme wakitanzania. Hakika m'bunifu wa hii Nembo kama alishapata tunzo basi anastahili nyengine. Ubunifu wake hauna utofauti na uvumbuzi wa Tanzanite kama watanzania inapaswa kujivunia kazi za wataalamu wetu badala ya kuzitafutia kasoro zisizokuwa za msingi. Najua kuna watu baadhi ya watanzania wenye maono ya hovyo ya kisiasa wanaweza kuhoji muonekano wa hii Nembo na licha ya vijisababu vyote vile vinavyotolewa kikubwa hapa kinachowaasha wanaotoa maneno kuhusu hii Nembo ni hii rangi ya kijani ya vivazi vilivovaliwa katika hii Picha.
ReplyDelete