Serikali Yapiga Marufuku Makanisa Yanayofanya Maombi Usiku

Serikali Yapiga Marufuku Makanisa Yanayofanya Maombi Usiku
Makanisa ambayo yanatoa huduma ya maombi nyakati za usiku yamepigwa marufuku na serikali nchini Kenya kufanya hivyo.



Serikali katika Kaunti ya Narok imesema kuwa maombi hayo yanapelekea mimba za utotoni kuongezeka wengi wao wakiwa ni wanafunzi.

Amri hiyo imetolewa na Kamishna wa Kaunti ya Narok, George Natembeya Ijumaa ya wiki iliyopota. Ambapo amesema kwa mujibu wa takwimu za Kaunti hiyo zinaonesha wastani wa wanafunzi 15 wanapata mimba kwenye kila shule katika kaunti hiyo.

Natembeya amesema kuanzia mwezi Machi hadi Aprili tayari wanafunzi 17 wamepata ujauzito katika shule ya wasichana ya Suswa, hii ni kwa mujibu wa taratibu za kuwapima mimba kila baada ya miezi miwili.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad