Serikali yawataka Wakurugenzi kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani


Serikali imewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote 185 zilizopo Tanzania bara kuhakikisha wanatoa asilimia 10 ya mapato ya ndani ili kuepukana na tabia ya kuwasababishia kuandikiwa deni kwenye taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali.

Naibu waziri wa Tamisemi Josephat Kakunda, ametoa kauli hiyo leo (Aprili 04, 2018) kwenye mkutano wa 11 unaoendelea kufanyika mkoani Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Susan Mgonukulima ambaye alitaka kujua asilimia 10 za mfuko wa halmashauri kwa vijana na wanawake una kiasi gani.

"Kumekuwa na changamoto za kiutekelezaji ambazo zimekuwa zikisababisha utekelezaji wa azimio hilo usifikie asilimia 100. Naziagiza Halmashauri zote 185 nchini kutoa asilimia 10 ya mapato halisi ya ndani kwa ajili ya mikopo kwa wanawake (asilimia 5) na vijana (asilimia 5)", amesema Kakunda.

Kwa upande mwingine, Naibu waziri wa Tamisemi Josephat Kakunda amesema endapo wakurugenzi hao hawatotenga kiasi hicho kilichotakiwa basi watachukuliwa hatua stahiki dhidi yao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad