Akizungumza na Risasi Jumamosi ikiwa ni siku chache baada ya video queen, Agness Gerald ‘Masogange’ kufariki dunia kisha kuagwa viwanjani hapo, Shilole alisema yeye anatoa agizo kuwa, ikiwa ametokea amefariki dunia leo au kesho, kama siyo kuagwa nyumbani kwake Gongo la Mboto, basi aagwe msikitini.
“Mimi sitapenda kabisa taratibu za mazishi yangu zifanyike katika Viwanja vya Leaders, ni bora kama nyumba yangu itakuwa haijamalizika basi watu wakafanyie taratibu hizo msikitini kwa sababu mimi ni mtoto wa kiislam, siwezi kuagwa kwenye viwanja ambavyo watu wanakunywa na kuuza pombe,” alisema Shilole.
SOMA Pia: Job Opportunity at Brighter Monday Tanzania, Marketing Intern