Umetimia mwaka mmoja tangu tukio la Roma, Moni na wenzao kutekwa na watu wasiojulikana.
Tukio hilo lilitokea April 05, 2017 siku kama ya leo wakati wasanii hao wakiwa ndani ya studio za Tongwe Records ambapo watekaji waliondoka na baadhi ya vifaa vya studio.
Tukio hilo bado lipo kichwani mwa msanii Moni ambaye leo hii amekumbushia kile kilichotokea. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
Siku kama ya leo mwaka 2017 watu wasiojulikana walikuja Studio na kujitambulisha kisha wakatubeba kama kuku.
Tulifungwa mikono na macho tukapelekwa umbali mrefu tukasimama sehemu watu wakanong’onezana kwa dakika 20 kisha tukapeleka kwenye nyumba ambayo tulikula kisago heavy mijeledi mateke na marungu kwa mara ya kwanza nilisali sala ya mwisho nikijua mwisho wangu umefika.
Roma, Moni na wenzao walipatikana April 08, 2017 taarifa zilizothibitishwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni kwa wakati huo, Abubakar Kunga, baada ya hapo walichukuliwa hadi kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya mahojiano.
Soma Pia; Wasanii watua nyumbani kwa RC Makonda, RC atoa ahadi hii kuhusu Roma
Pia siku ya leo Roma amekabidhiwa cheti cha usajili kutoka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), hii ni baada ya kupewa masharti ya kufanya hivyo na Wizara ya Habari ili aweze kufutiwa adhabu yake ya kutojihusisha na muziki kwa miezi sita.
Siku Kama ya Leo Roma na Wenzake Walitekwa na Wasiojulikana, Moni Akumbushia .... Asimulia Ilivyokua
0
April 05, 2018
Tags