Simba Waendelea Kutoa Dozi Okwi, Bocco Wazidi kung'aa

Simba Waendelea Kutoa Dozi Okwi, Bocco Wazidi kung'aa
Vinara wawili wa mabao kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara ambao pia ni washambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi na John Bocco wamefunga mabao mawili leo na kuipa ushindi Simba dhidi ya Tanzania Prisons.


Simba wameendelea kuhifadhi mwendelezo wao wa kutopoteza mchezo kwenye ligi msimu huu baada ya kuiadhibu Prison mabao 2-0 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam jioni hii.

Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco dakika ya 35 ambaye sasa amefikisha mabao 14 msimu huu huku bao la pili likifungwa na Emmanuel Okwi kwa njia ya penati dakika ya 80 na kumfanya sasa afikishe mabao 19.

Baada ya ushindi wa leo Simba sasa imefikisha alama 58 katika michezo 24 ya ligi msimu huu hivyo kuendelea kujikita kileleni ikiwakimbia wapinzani wao Yanga ambao wapo katika nafasi ya pili wakiwa na alama 47.

Simba iko mbele ya Yanga kwa michezo miwili ambapo Yanga inayowakilisha taifa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho imecheza mechi 22 pekee hivyo ikishinda viporo vyake inaweza kufikisha alama 53.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad