Sipelekeshwi na Mapenzi na Wala Sijawahi Kumlilia Mwanaume- Nisha

Sipelekeshwi na Mapenzi na Wala Sijawahi Kumlilia Mwanaume- Nisha
Baada ya kuanzisha drama la aina yake hivi karibuni na kuingia katika headline na aliyekuwa Boy Friend wa J kwa kile kilichodaiwa walikuwa mapenzini, muigizaji Nisha amesema hajawahi kupelekeshwa na mapenzi.

Mingizaji amesema video zilizotoka katika mitandao zikimuonyesha akilia si kwa sababu ya mapenzi kama ilivyokuwa ikielezwa bali ni promotion ya ngoma yake ‘Bachela’.

“Yes, sijawahi kumlilia mwanaume yeyote, kipindi ambacho naanza kuposti nalia ndio kipindi ambacho tupo production, ukiusikiliza ule wimbo kuna sehemu natakiwa niwe nalia na ndio promotioni yangu ya kwanza kuiposti Instagram,”  Nisha ameiambia Times FM.

“No! no! hakuna binadamu ambaye hajawahi kuumizwa kwenye mapenzi ila sasa hivi nimeshakuwa mkubwa ambapo moyo wangu umeshashonwa vizuri unajielewa zaidi unaweza kuji-control na sipelekeshwi na mapenzi,” amesema.

Muigizaji huyo kutoka industry ya Bongo Movie kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Bachela.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad