Hayo yameelezwa leo Aprili 12 bungeni na Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyesema kuwa habari iliyochapishwa Aprili 9 ilidhamiria kuchafua hadhi ya bunge.
Hayo yamekuja baada ya mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga kuomba mwongozo wa Spika juzi Aprili 9, akihoji iwapo habari iliyoandikwa na gazeti hilo yenye kichwa cha habari “Bunge linajipendekeza?” haidhalilishi bunge.
Spika Ndugai leo Aprili 12, ameliambia bunge kuwa mwandishi huyo na wahariri watatakiwa kuhojiwa na kamati hiyo ya bunge.
