Suala la Tsh. Trilioni 1.5 Professor Jay alipeleka kwa Mhe. Shonza

Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’ amehoji sababu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kumiliki viwanja vikubwa vya michezo wakati kuna uwaba wa viwanja hivyo kwa wanamichezo.

Akiuliza swali Bungeni leo April 23, 2018 amesema tatizo la wanamichezo wa Tanzania ni viwanja kukosa ubora na anafikiri Tsh. Trilioni 1. 5 (zinazodaiwa kupotea) zingeweza kupunguza changamoto hiyo.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema sera ya michezo ya mwaka 1995 inahamasishwa wadau, vyama, taasisi kumiliki viwanja vya michezo.

“Kwa hiyo viwanja vyote vinamilikiwa kwa uhalali, ni haki yao na hakuna kiwanja hata kimoja kimeporwa na Chama cha Mapinduzi,” amesemaMhe. Shonza.

Utakumbuka April 20, 2018 wakati Rais Magufuli akiwaapisha majaji Ikulu Dar es Salaam alisema katika ripoti aliyopokea kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad haikuwa na upotevu wa fedha Tsh. Trilioni 1.5 kama inavyodaiwa bali ni watu wanatumia uhuru wao vibaya na kupotosha kitu kilicholeta taharuki.

Bongo5
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad