Kocha Mkuu wa klabu ya Mbao FC Mrurundi, Etiene Ndayiragije huwenda akaingia mkataba wa muda na mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara Young Africans kufuatia timu hiyo kukosa huduma ya George Lwandamina aliyekwenda kwao Zambia.
Taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kuwa kocha huyo wa Mbao, Ndayiragije anahusishwa kujiunga na Yanga SC kurithi mikoba ya Lwandamina aliyetangazwa rasmi kutoka ndani ya klabu ya Zesco United, Aprili 10
Aprili 11 mwaka huu Kocha, Etiene Ndayiragije alikosekana kwenye eneo la benchi la ufundi la timu ya Mbao FC wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania Bara raundi ya 24 wakiwa nyumbani licha ya kuchomoza na ushindi wa mabao 2 – 1 dhidi ya Njombe Mji jambo ambalo likaongeza uvumi wa kutua Yanga SC.
Moja ya chombo cha habari kimepata kumhoji, Etiene Ndayiragije juu ya tetesi hizi za kutakiwa kujiunga na mabingwa hao wa tetezi wa ligi ya Vodacom, Yanga SC na kusema kuwa hupokea taarifa kutoka kwa wasimamizi wake ‘management’ pale jambo linapo kamilika na sio tetesi na kwakuwa hajaambiwa chochote anaamini kuwa dili hilo halikukamilika.