Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limesema kuwa imani yao kwa Yanga ni kubwa na wanaamini timu hiyo itaibuka na matokeo mazuri kwenye mchezo wa marudiano kesho dhidi ya Welayta Dicha.
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi, amebainisha hayo leo, ambapo amesema Yanga inaweza kuitoa Woilata Dicha, kama watatumia tena udhaifu ulioonekana kwa wapinzani hao, kwenye mchezo wa kwanza.
''Yanga ni timu bora na walionesha hilo kwenye mchezo wa kwanza kwa kuwafunga Dicha mabao 2-0 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam hivyo tuna imani kubwa sisi kama shirikisho Yanga watalinda ushindi wao na kusonga mbele hatua ya makundi'', amesema.
Madadi ameongeza kuwa kocha wa Yanga aliyeondoka George Lwandamina amepata CV nzuri akiwa na klabu hiyo, kwa hiyo si jambo geni kwa makocha wa nje kuondoka pale wanapopata mafanikio Tanzania.