TMA Tatoa Tahadhari ya Mvua Kubwa Zinazotarajiwa Kunyesha Nchini

TMA yatoa tahadhari kubwaMamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo yote ya pwani kuanzia leo usiku mpaka Aprili 16 mwaka huu.


Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Ijumaa) na kudai kutakuwepo vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 katika saa 24 ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Aidha, TMA imewashauri wakazi wa maeneo yaliyotajwa kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zinazotolewa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad