MBUNGE wa Singi da Mashariki (Chadema), Tundu Lissu
amesema kwa amara nyingine tena, leo Aprili 11, 2018 ataingia kwenye
chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa oparesheni ya mguu wake wa
kulia ambao bado una matatizo kutokana na risasi alizopigwa Septemba 7 mwaka jana nyumbani kwake, Area D, Dodoma.
Upasuaji huu utakuwa ni wa 20 tangu alipoanza kutibiwa, baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka jana.
Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji kwa
matibabu amesema kwamba oparesheni hiyo ni sehemu ya tiba ya mguu huo
huku akieleza kuwa kwenye mikono yuko salama kitabibu.