Mkataba huo umesainiwa leo katika mkutano uliofanyika ndani ya studio za Azam TV jijini Dar es Salaam, ambapo kampuni hiyo imewakilishwa na Ofisa Uhusiano wake Nembris Soka.
Tukio pia limeshuhudiwa na mwandishi na muongozaji wa filamu hiyo, Neema Ndepanya.
Kwa upande wa Wema amesema tangu kutolewa rasmi kwa filamu hiyo, wapenzi wake wamekuwa wakiipata kupitia ‘Application’ ya Wema Sepetu, na hapakuwa na DVD zozote ambazo zilikuwa zikisambazwa kwa watu.
Amesema kampuni hiyo imeamua kufanya kazi hiyo baada ya filamu hiyo kushinda tuzo mbili katika Tuzo za Kimataifa za Filamu (SZIFF) zilizofanyika Aprili MOSI, mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City.
Soka yeye amesema Kampuni ya Auguster wamevutiwa na kiwango cha filamu hiyo na wameona jinsi mashabiki wa filamu nchini walivyo na kiu ya kuitazama filamu hiyo, na ndiyo maana wameamua kuifanya kazi hiyo ya usambazaji ili iwafikie watu.