Ubungo Yatenga Bilioni 1.9 kwa Mikopo ya Wakina Mama na Mikopo

Ubungo Yatenga Bilioni 1.9 kwa Mikopo ya Wakina Mama na Mikopo
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 1.9 kwa ajili ya mkopo kwa kina mama na vijana.

Hayo yamesemwa leo, April 18, 2018 na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Mhe Boniface Jacob wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano na benki ya CRDB ambapo mikopo hiyo itatolewa kupitia benki hiyo.

Meya Jacob ametoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo kwani idadi yao imeonekana kuwa ndogo kwani mfuko huu ni nusu kwa vijana na nusu kwa kina mama na asilimia 20 inakwenda kwa walemavu.

“Nikiwa Manispaa ya Kinondoni tuliweza kutenga 800M kwa ajili ya mikopo kama hii, lakini Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ina muda wa mwaka mmoja na nusu tu lakini unaweza kuona kiasi tulichotenga kwa ajili ya mikopo kwa vijana na kinamama, ni kwa sababu tuko commited kuwasaidia wananchi wa Manispaa ya Kinondoni” amesema Meya Boniface Jacob.

Manispaa ya Ubungo itakuwa ya kwanza kwa utekelezaji wa agizo kwamba asilimia 20 ya fedha ni kwa ajili ya walemavu. Kwa taarifa ya mratibu wa zoezi hilo, Wanawake waliojitokeza ni 11,321, vijana idadi yake ikiwa ni 1124.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad