Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa atampeleka Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi(TSNP), Abdul Nondo Uhamiaji ambapo jana alipelekwa katika ofisi hizo kwaajili ya kuhojiwa uraia wake.
Zitto kupitia mitandao yake ya kijamii amesema kuwa Idara ya uhamiaji imekuwa ikitumika kisiasa dhidi ya mwanafunzi huyo na sio kosa hata kidogo Abdul Nondo kuzaliwa Kigoma Ujiji.
Nitampeleka Abdul Nondo Uhamiaji tarehe 20/4/2018 kwa mamlaka yangu kama Mbunge wa Kigoma Mjini ( Jimbo analotoka Abdul na wazazi wake na mababu zake).
Idara ya Uhamiaji inatumika kisiasa dhidi ya mwanafunzi Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania. Sio kosa hata kidogo Abdul kuzaliwa Ujiji Kigoma. Imekuwa tabia ya Serikali kuwapa kesi za uraia watu wanaotoka mikoa ya magharibi hasa Kigoma. Suala la Nondo ni vita dhidi ya Watu wa Kigoma. Tutapambana. Tutampigania Abdul Nondo. Watanzania tusikubali upuuzi huu wa watu wa Uhamiaji na Serikali ya Awamu ya awamu ya Tano kuwafanya raia wa mikoa kama Kigoma kuwa raia wa daraja B
Uhamiaji Inatumika Kisiasa Dhidi ya Abdul Nondo Sio Kosa Kuzaliwa Kigoma –Zitto Kabwe
0
April 05, 2018
Tags