Unatafuta Mwenzi wa Maisha Yako? Soma Hii Inakuhusu Sana

Ni kawaida watu kudhani kwamba kama zawadi imefungwa kwa kabrasha au mfuko au package nzuri sana basi kilichomo ndani kitakuwa ni kitu chenye thamani kubwa sana na kizuri sana.

Ukweli ni kwamba ufungaji wa zawadi au uzuri wa material yanayotumika kufunga zawadi haviwezi kukwambia uhakika wa uzuri wa kitu kilichomo ndani, badala yake unahitaji kufikiria zaidi, au kufanya utafiti zaidi ya hayo makabrasha ya kufungia zawadi ili kujua kilichomo ndani.

Linapokuja suala la mahusiano, hasa mahusiano mapya, watu wengi huwaangalia partners wao kwa nje bila kuangalia undani wa mtu mwenywe ili kujua ndani kuna kitu gani.
Wengi huvutiwa na uzuri wa nje au sifa za nje badala ya kuangalia na kuchunguza kile kilichomo ndani ya huo uzuri.
Watu hawaoni sababu ya kuchunguza au kutumia muda kupata ukweli na matokeo yake ni kujuta mbele ya safari.

Siku hizi si ajabu ukakuta mtu ameshakubaliana na mtu hadi kufika hatua ya mbali sana katika mahusiano bila hata kujua majina yote mawili ya mtu ambaye anasema anampenda na kwamba bila yeye anaona maisha hayana maana.
Watu wanafahamiana na baada ya mwezi tayari wanakubaliana kuoana na kuwa mke na mume.

Unahitaji ku-dig deeper linapokuja suala la mahusiano,
Utajiri, Kujulikana, Cheo, Urembo, Uzuri wa ngozi,
Familia yenye uwezo, Vipaji, Usomi, Umaskini au
kitu chochote cha nje ni sawa na kabrasha ambalo linatumika kuibeba zawadi yenyewe.

Inaweza kuwa zawadi ni makaratasi na matambala tu yamewekwa humo na utakapokuja kugundua unakuwa umeshachelewa kabisa na matokeo yake kujuta.
Umeuziwa mbuzi kwenye gunia.
wakati unao fikiria kwa makini

Kawaida kama unatafuta uhusiano wa kudumu ni vizuri uka-invest muda mwingi kuhakikisha unamfahamu mtu vizuri, moyo wake
(marry the soul not the skin).

Maisha tunapoishi hupelekea mabadiliko ya sifa za nje, watu hufirisika, watu hunyonyoka nywele, watu huzeeka, watu hupata stress, watu huwa vilema, watu hunenepeana, watu huugua, watu hubadilika, watu hukonda hata wakawa tofauti na walivyo labda wakati wa kuanza urafiki wenu muwe mmekubaliana kwamba yakitokea mabadiliko tu kila mtu aanze mbele au achukue chake, ndo maana leo ndoa ni kama watu wanaoenda shopping
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad