Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe atakapokuwa akijibu hoja za wabunge zilizotolewa katika mjadala wa bajeti hiyo mwaka 2018/19, kueleza sababu za kuufungia wimbo wa Mwanaume mashine.
Akizungumza bungeni leo Aprili 27, Zungu amesema wimbo wa Mwanaume mashine unamtaja mcheza soka wa timu ya Simba, Ramadhani Kichuya.
“Wimbo huo unamtaja mchezaji soka wa timu ya Simba, Ramadhan Kichuya, wapenzi wa timu hiyo wangependa kuusikiliza siku ya Jumapili wakati Simba ikipambana na Yanga katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,” amesema Zungu.