Viongozi wa ZFA Wakalia Kuti Kavu Baada ya Kufungiwa CECAFA

Viongozi wa ZFA Wakalia Kuti Kavu Baada ya Kufungiwa CECAFA
Baada ya Karume Boys kufungiwa na CECAFA, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake ya Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo imesema kama viongozi wa ZFA watapatikana na kosa basi wajiandae kukaa kando.


Katibu mkuu wa Wizara hiyo Omar Hassan (King) amesema ikithibitika kuwa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) wao ndio wenye makosa mpaka Karume Boys wakaondolewa katika mashindano basi wajiwajibishe wenyewe kwa kujiuzulu.

"Kama itakuwa kosa lao ZFA na kama na mimi nimo ZFA basi nitakaa pembeni, naamini na wao wenyewe watatumia busara ya hali ya juu kukaa pembeni kupisha watu wengine watimize majukumu kama wao yamewashinda", amesema Mh. Omar.

Zanzibar iliondolewa katika mashindano ya CACAFA kwa vijana wa umri chini ya miaka 17 yanayoendelea nchini Burundi kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo kanuni ya mashindano iliwataka wachezaji waliozaliwa kuanzia 01/01/2002.

Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholaus Musonye alisema kuwa ZFA walitumiwa ufafanuzi wa umri kwenye Barua Pepe ya shirikisho hilo labda kama hawakusoma.  Karume Boys imepewa adhabu tatu ikiwemo kuondolewa mashindanoni, na faini dola 15,000 (Sh 30 milioni).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad