Vodacom M-Pesa Yapewa Tuzo na Kutambuliwa na GSMA Kwa Huduma Zilizotukuka

Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya M-PESA
imetambuliwa na kupatiwa cheti kutambua ubora uliotukuka wa huduma za
kifedha. Tuzo hii imetolewa jana jijini Abidjan, Côte d’Ivoire kutambua usalama
na uhakika pamoja na nia thabiti ya M-Pesa katika kulinda haki ya mteja.

Tuzo hii imetolewa bada ya Vodacom Mpesa kufiika vigezo vilivyowekwa na
GSMA ambavyo ni viwango vya juu vya kulinda amana ya mteja, usalama wa
huduma, usiri na kulinda taarifa za mteja, kupambana na utakatishaji fedha,
kupambana na wanaogharamia vikundi vya ugaidi, na pia kupambana na
mbinu zote za udanganyifu.

Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom anasema “Utambuzi na cheti
hiki vinathibitisha nia na utendaji wa Vodacom Tanzania katika kuhudumia na
kulinda haki za mteja katika eneo lote la biashara ya MPesa, tukiwa ni
mtandao unaoongoza kwa huduma ya pesa cheti hiki kitatupatia nafasi ya kuaminika zaidi na kutuongezea ari ya kiutendaji ili kuwaridhisha wateja wetu
ambao wametufanya kuwa kampuni ya simu ya kwanza nchini kupata
utambulisho huu baada ya kufikia vigezo, alisema Ian Ferrao, Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom.

Cheti hiki cha GSMA kimekuja wakati ambapo Vodacom Mpesa inatimiza
miaka 10 ya M-pesa Tanzania. Kwa takribani miaka 10 sasa M-pesa imeweza
kubadilisha maisha na kuipandisha Tanzania kiuchumi kupitia huduma za
kutuma na kutoa fedha, malipo ya bili, akaunti za kutunza fedha, mikopo na
mengineyo mengi. M-pesa leo ina zaidi ya wateja milioni 8, wakala 106,000,
biashara za kawaida zaidi ya 2000, wafanyabiashara wakubwa zaidi ya
15,000, benki zilizounganishwa zaidi ya 30. Kupitia huduma zake M-pesa
imewezesha wakazi wa kitanzania wa mijini na vijijini kuwa sehemu ya mfumo
mzima wa kiuchumi unaotambulika,pamoja na ongezeko kubwa la kiuchumi
katika jamii nyingi za kitanzania.Mfumo huu rasmi nchini Tanzania umekuza
uchumi kwa mwaka 2017 hadi kufikia 65% kutokea 58% mwaka 2013 na 44%
kwa mwaka 2009 Mwaka mmoja baada ya M-pesa kufunguliwa rasmi nchini
Tanzania.

VIDEO:

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad