Wakimbiaji wa Kike Wenye Homoni za Kiume Kama Caster Semenya Wabanwa na Kanuni Mpya za Riadha Duniani

Baadhi ya wakimbiaji wa kike wenye homoni nyingi za kiume watatakiwa kukimbia dhidi ya wanaume au kubadili mashindano mpaka pale watakapopata matibabu, hizi ni sheria mpya zilizotolewa na chombo cha riadha duniani.

Sheria, ambazo zitaanza kutumika tarehe 1 mwezi Novemba,zitawahusu wanawake wanaokimbia kuanzia mita 400 mpaka maili moja

Mshindi wa mbiao za mita 800 kwenye michuano ya Olimpiki, Caster Semenya ni miongoni mwa watakaoathirika

Mkimbiaji wa Afrika Kusini awali alitakiwa kufanyiwa kipimo cha kubaini jinsia na wakuu wa shirika hilo laini majibu hayakuwekwa hadharani.

''Sheria hizo si kuhusu udanganyifu, ni kuhakikisha kunakuwa na michuano ynayofanyika kwa haki na umaana''Rais wa IAAF Lord Coe alieleza

akizungumza baada ya kushinda mbio za mita 800 na mita 1500 kwenye michuano ya jumuia ya madola mwezi Aprili,Semenya alisema atakimbia umbali mrefu zaidi

Wanariadha wanawake wanaotaka kushindana wanalazimika kupata dawa kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kuingia mashindanoni, na kuhakikisha kuwa kiwango cha homoni hizo kinashuka.

Ikiwa mwanariadha wa kike hatataka kutumia dawa, wanaweza kushindana kwenye:

Mashindano yeyote ya kimataifa isipokuwa mbio za mita 400 na maili moja
Michuano yeyote ambayo sio ya kimataifa
michuano ya wanaume katika ngazi yeyote
michuano inayohusisha watu wenye jinsia mbili
Wanaotaka kushiriki michuano hawatakiwi kufanyiwa upasuaji .

Taarifa ya IAAF imesema sheria hizo ''hazina lengo la kuwahukumu au kuhoji jinsia ya mwanariadha''.

Katika utafiti wa hivi karibuni imeonekana kuwa wanawake wenye mchanganyiko wa homoni za kiume wana uwezo mkubwa wa kukimbia zaidi ya wasio nazo.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad