Wagonjwa wawili kati ya wanne waliopandikizwa figo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wameruhusiwa leo baada ya afya zao kuimarika.
Akizungumza leo Aprili 28, Mkuu wa Kitengo cha Figo, Dk Jackline Shoo amesema upandikizaji huo ni hatua kubwa na imedhihirisha kuwa madaktari wa Tanzania wanaweza.
Dk Shoo amesema wagonjwa wote waliopandikizwa wanaendelea vizuri ila wamewaruhusu wawili huku wakiendelea kuwafuatilia waliosalia.
"Tunashukuru serikali kwa kutuwezesha tunaomba iendelee kutuona ili wigo wa huduma zetu upanuke, tuwahudumie hata watu kutoka nje ya nchi," amesema
Amesema ni matamanio yake kuona kitengo cha figo, kinakuwa na uwezo wa kuwahudumia watu wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.